PlaneteAfrique
Déconnexion


JK aweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara Mkoani Pwani

 JK aweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara Mkoani Pwani


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Jakaya Kikwete ameweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya Msata – Bagamoyo na kuwataka  wakazi wa mkoa wa Pwani kutumia fursa zinazotokana na barabara hiyo kujiletea maendeleo.



Rais Kikwete amesema barabara hiyo itakapokamilika ujenzi wake kwa kiwango cha lami itafungua milango ya biashara kwa wakazi wa mkoa wa Pwani pamoja na kupungunza tatizo la foleni katika barabara ya morogoro.



Rais Kikwete aliwasili katika kijiji cha kiwangwa kuweka jiwe la msingi ujenzi wa kilometa 64 za barabara ya  msata –bagamoyo kwa kiwango cha lami na akatumia fursa hiyo kuwaasa wakazi wa mkoa wa Pwani kutumia barabara hiyo kujiletea maendeleo.



Halikadhalika Rais Kikwete amezungumzia tatizo la watu wanaovamia na kujenga nyumba katika hifadhi ya barabara kuwa katu hawatalipwa fidia na badala yake watakaolipwa fidia ni wale tu ambao watabainika kuwa barabara iliwakuta.



Mapema akimkaribisha Rais Kikwete kwenye sherehe hizo, waziri wa ujenzi Dokta John Magufuli ameiomba bodi ya wakandarasi nchini kuichukulia hatua kampuni  iliyopewa zabuni ya kufanyia tathmnini ujenzi wa barabara hiyo kwa kuifanya kwa kiwango cha chini jambo ambalo limeisababishia serikali hasara kubwa.



Mkuu wa wakala wa ujenzi wa barabara nchini injinia Patric Mfugale amesema ujenzi wa kilometa 64 za barabara ya Msata Bagamoyo unagharimu shilingi bilioni 90 fedha ambazo zimetolewa na serikali ya Tanzania ambapo hadi sasa kilometa 37 zimekamilika.



Joseph Chewale, TBC Pwani.




Last Updated ( Wednesday, 19 September 2012 12:52 )


 
Publicateurs
Devenez publicateur Partagez votre voix Racontez l'Afrique qui bouge

Touchez plus de 0 milliard d'Africains

Devenir publicateur →
Partager Partager

À lire aussi

TANZANIE
Getty Images On Friday, Walmart announced it will close 269 stores globally as it struggl...
1/26/2016 -  8057
TANZANIE
A major search is under way in the south of Iraq’s capital, Baghdad, after the kid...
1/26/2016 -  5719
TANZANIE
China’s Dalian Wanda Group will buy a controlling stake in Hollywood film studio Legendary Ent...
1/14/2016 -  5579
TANZANIE
There has been an explosion in a district of Istanbul popular with tourists, reports say, with sever...
1/14/2016 -  5446
TANZANIE
US President Barack Obama is to widen background checks on buyers of firearms, in a series of measur...
1/5/2016 -  5766
TANZANIE
Don’t let her diminutive size fool you: Kendall Jones, a cheerleader at Texas Tech, has faced ...
7/2/2014 -  3849
TANZANIE
Don’t let her diminutive size fool you: Kendall Jones, a cheerleader at Texas Tech, has faced ...
7/2/2014 -  3733
TANZANIE
Vice-President Mohamed Gharib Bilal has directed the Ministry of Tourism and Natural Resources to do...
6/25/2014 -  3931
TANZANIE
French club Valenciennes FC is interested in signing Rwanda international defender Salomon Nirisarik...
6/4/2014 -  3924
TANZANIE
UK yacht design studio Claydon Reeves has created a vessel billed as one of the fastest and most ele...
5/28/2014 -  4232
TANZANIE
Tanzania Women’s Bank Limited (TWB) has forged business links with Tanzanians in the Diaspora who wa...
5/21/2014 -  3460

TANZANIE - accès rapides

Actualités par pays

 

Newsletter


 
 
 
 
 
 

Actualités par pays

TANZANIE - accès rapides

Newsletter


 
 
 
 
 
MySite
WS-MYSITE
✨ Présence web
Créez votre site clé en main
Démarrer →