PlaneteAfrique
Déconnexion


Ukosefu fedha wachangia kuzorotesha kilimo nchini



Imeelezwa kuwa tatizo la ukosefu wa uwezeshaji kifedha katika  sekta ya kilimo umekuwa ukichangia kuzorotesha maendeleo ya sekta ya kilimo nchini



Tafiti iliyofanywa na taasisi ya masuala ya kiuchumi na kijamii ESRF ya mwaka 2011 imebainisha  kuwa sekta ya kilimo imekuwa ikishuka kwa kiasi kikubwa kutokana na upatikanaji hafifu wa masoko, ukosefu mkubwa wa taaluma ya kilimo cha umwagiliaji hali kadhalika uwepo wa miundo mbinu duni ya uzalishaji wa sekta ya kilimo



Akitoa taarifa hiyo mjini Unguja kwa wadau wa sekta ya kilimo kutoka taasisi mbalimbali za serikali, mtafiti mkuu wa masuala ya sekta ya kilimo kutoka taasisi hiyo Dkt  Oswald  Mashindano  amesema  tafiti  walizoweza kuzifanya  katika ukanda wa Kusini,Kaskazini  na Mashariki mwa  Tanzania umeonyesha dhahiri wakulima  wengi wanashindwa kuzalisha kwa kiasi kikubwa kutokana na matatizo mbalimbali yanayowapelekea  kushindwa  kufikia malengo ya kukiona kilimo ni sekta muhimu katika ukuaji wa maendeleo yao ya kiuchumi hali kadhalika maendeleo  ya taifa kwa ujumla.



Hatahivyo amesema bado ukulima  unaofanyika hivi sasa haujaweza  kubadilika na kuendelea  kutumia Kilimo  cha jembe la mkono suala ambalo  sekta hiyo inazidi  kuporomoka.



Ameongeza  kuwa tatizo lingine ambalo  linawafanya wakulima  wengi kushindwa kusonga  mbele ni ukosefu mkubwa wa uwezeshaji wa rasilimali fedha  suala  ambalo  nalo limekuwa ni changamoto kubwa kwa upande wao .



Baadhi ya wadau waliokuwa katika mdahalo huo wa kujadili tafiti hiyo  wamesema kuwa umuhimu mkubwa  kwa serikali na  sekta binafsi kuangalia  uwezekano wa kuwawezesha zaidi  wakulima  kifedha  hali kadhalika na upatikanaji wa masoko ndani na nje ya  nchi.



Utafiti  huo umeonyesha kuwa  asilimia  sabini  hadi  themanini  ya watu wengi  wamo katika  sekta ya Kilimo  kati ya hao  asilimia  86.5  ni wakina mama  lakini  bado  sekta ya Kilimo haijaweza  kufikia malengo  ya uzalishaji mkubwa.



Kulthum Ali, TBC Zanzibar. 




Last Updated ( Friday, 13 September 2013 13:03 )


 


Publicateurs
Devenez publicateur Partagez votre voix Racontez l'Afrique qui bouge

Touchez plus de 0 milliard d'Africains

Devenir publicateur →
Partager Partager

À lire aussi

TANZANIE
Getty Images On Friday, Walmart announced it will close 269 stores globally as it struggl...
1/26/2016 -  8058
TANZANIE
A major search is under way in the south of Iraq’s capital, Baghdad, after the kid...
1/26/2016 -  5721
TANZANIE
China’s Dalian Wanda Group will buy a controlling stake in Hollywood film studio Legendary Ent...
1/14/2016 -  5580
TANZANIE
There has been an explosion in a district of Istanbul popular with tourists, reports say, with sever...
1/14/2016 -  5447
TANZANIE
US President Barack Obama is to widen background checks on buyers of firearms, in a series of measur...
1/5/2016 -  5767
TANZANIE
Don’t let her diminutive size fool you: Kendall Jones, a cheerleader at Texas Tech, has faced ...
7/2/2014 -  3850
TANZANIE
Don’t let her diminutive size fool you: Kendall Jones, a cheerleader at Texas Tech, has faced ...
7/2/2014 -  3734
TANZANIE
Vice-President Mohamed Gharib Bilal has directed the Ministry of Tourism and Natural Resources to do...
6/25/2014 -  3932
TANZANIE
French club Valenciennes FC is interested in signing Rwanda international defender Salomon Nirisarik...
6/4/2014 -  3925
TANZANIE
UK yacht design studio Claydon Reeves has created a vessel billed as one of the fastest and most ele...
5/28/2014 -  4233
TANZANIE
Tanzania Women’s Bank Limited (TWB) has forged business links with Tanzanians in the Diaspora who wa...
5/21/2014 -  3462

TANZANIE - accès rapides

Actualités par pays

 

Newsletter


 
 
 
 
 
 

Actualités par pays

TANZANIE - accès rapides

Newsletter


 
 
 
 
 
Nouveau

WS-Webzine

Publiez vos actualités et articles en ligne facilement.

  • Éditeur intuitif
  • Référencement optimisé
Découvrir →